Machapisho ya Kibunifu
Machapisho ya Kubunifu ambayo yamefanywa na Dkt. BabusaNovela Za Msururu Wa Makumba
Msururu wa Makumba ni novela tano za sayansi ambazo zimechapishwa na Queenex Publishers mwaka 2018. Novela hizi zinahusu safari za kisayansi za mhusika Makumba na babu yake wakitalii sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu, mimea, anga na nyinginezo kwa kutumia GAJABU....
read moreKijiji cha Ukame
Kijiji cha Ukame ni novela ya kiwango cha darasa la sita. Imechapishwa na shirika la Storymoja mwaka 2017. Ni ya kwanza katika msururu wa novela kuhusu mhusika BINTI KITABU ambaye ni msichana anayetumia nguvu za kiajabu za vitabu kusuluhisha matatizo ya jamii. Katika...
read moreVazi la Mhudumu
Vazi la Mhudumu na Hadithi Nyingine kutoka Afrika Mashariki ambayo imehaririwa na P.I. Iribemwangi na Hamisi Babusa ni diwani ya hadithi fupi iliyochapishwa na EAEP mwaka 2016. Ni diwani inayojumuisha hadithi za kuvutia zilizoandikwa na waandishi kutoka Kenya,...
read moreNuru ya Kiza
NURU YA KIZA ni tamthilia ya Kiswahili. Imechapishwa mwaka 2016 na shirika la EAEP. Inahusu Mkulu kabaila Kabwela. Kabaila Kabwela (KK) ni Mkulu wa nchi ya Matopeni. Siku moja anaamua kutathmini utendakazi wa maliwali wake aliowapa majukumu mbalimbali ya uongozi...
read moreSina Zaidi Na Hadithi Nyingine
Sina Zaidi Na Hadithi Nyingine (Wahariri) P.I. Iribe Mwangi na Ken Walibora Hii ni diwani ya Hadithi Fupi Ambayo Imechapshwa na Target Publishers mwaka wa 2011. Hamisi Babusa amechangia hadithi moja (Shajara ya Mheshimiwa) katika Diwani hii. Shajara ya Mheshimiwa...
read moreCheupe na Cheusi
Hii ni Novela inayolenga wanafunzi wa darasa la nne. Inahusu msichana mrembo aliyeitwa Cheupe na masaibu aliyoyapitia mikononi wa mamake wa kambo na dadake wa kambo Cheusi. Novela hii ilichapishwa mwaka wa 2013 na Oxford University Press, Nairobi....
read moreGitaa na Hadithi Nyingine (Mhariri) Timothy Arege
Gitaa na Hadithi Nyingine ni Diwani ya hadithi Fupi iliyochapishwa na Longhorn Publishers mwaka wa 2011. Hamisi Babusa alichangia hadithi Mbili za kusisimua katika huu mkusanyiko. Alichangia Jana si Leo na Maendeleo.Jana si leo inahusu kijana Musa ambaye alikuwa na...
read moreWaja Leo Diwani ya Mashairi (Mhariri) Ken Walibora
Hii ni Diwani ya Mashairi iliyochapishwa na Oxford University Press mwaka 2012. Hamisi Babusa alichangia mashairi manne kwenye Diwani hii ambayo ni Hapo Hapo Pa Mawimbi Ninalipa Uzeeni, Mngojee Chini, Mla kwa Miwili na Afadhali Dooteni. Yote ni mashairi yenye ujumbe...
read moreKunani Marekani? Na Hadithi nyingine (Mhariri) P.I. Iribe Mwangi
Hii ni Diwani ya hadithi ambayo imechapishwa na Target Publishers mwaka 2011. Hamisi Babusa alichangia Hadithi moja inayoitwa Mtego wa Panya. Mtego wa Panya ni Hadithi kuhusu kijakazi wa nyumbani aliyeambukiza familia nzima virusi vya HIV. Kwa maelezo zaidi tafuta...
read moreMiali ya Ushairi
Hii ni Diwani nyingine ya Mashairi ambayo imechapishwa na EAEP mwaka 2015. Hamisi Babusa amechangia mashairi sita katika Hii Diwani. Mashairi yenyewe ni: Ukijigeuza Chano, Watu Watakufulia, Soma Somato Msoma, Mvumilivu, Kaida Fundi Mbaya, Jogoo la Shamba Haliwiki...
read moreMaskini Milionea na Hadithi Nyingine (Mhariri) Ken Walibora
Hii ni Diwani ya Hadithi Fupi Ambayo Imechapishwa na Oxford University Press mwaka 2012. Hamisi Babusa alichangia Hadithi moja ambayo pia ndiyo Anuani ya Kitabu. Masikini Milionea ni hadithi inayuhusu Kijana ambaye baada ya kuhafili chuoni alitafuta kazi bila...
read moreSauti Ya Shangwe
Hii ni Diwani ya Mashairi ambayo imehaririwa na Hamisi babusa. Washairi waliochangia mashairi Katik Hii Diwani ni Alamin Somo, Ahmed Hussein na Sheikh Nabhany. Diwani Hii ilichapishwa mwaka 2011. Mhariri Hamisi...
read moreMazingira
Hamisi Babusa alitunga Utenzi huu Unaohusu Madhara ya Kuharibu mazingira Na jinsi ya Kuyahifadhi. Aliandika Utenzi huu alipokuwa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo kikuu cha Kenyatta. Utenzi Huu ulioandikwa kwa Lugha sahili, umechapishwa mwaka 1995 na Phoenix...
read moreWakala na Waberu (INATOKA KARIBUNI!)
Novela hii bado iko jikoni inapikwa na itatoka karibuni. Ni simulizi kuhusu Uhusiano wa kimapenzi na kihasama wa Mkala na nduguye pacha Mberu. TAZAMA HUU UKURASA KARIBUNI KWA MAELEZO...
read more