Vazi la Mhudumu na Hadithi Nyingine kutoka Afrika Mashariki  ambayo imehaririwa na P.I. Iribemwangi na Hamisi Babusa ni diwani ya hadithi fupi iliyochapishwa na EAEP mwaka 2016.

Ni diwani inayojumuisha hadithi za kuvutia zilizoandikwa na waandishi kutoka Kenya, Tanzania, Zanzibar na Uganda waliobobea na wale wanaochipukia katika utanzu wa hadithi fupi.

Diwani hii inashughulikia maudhui mbalimbali kama vile elimu, siasa, ukabila, hadaa, mapenzi na unyumba, ushirikina na mengine anuwai. Waandishi wa hadithi zilizomo katika mkusanyiko huu wamezingatia kaida zinazobainika za utanzu wenyewe. Ni hadithi zinazotoa ujumbe wa wazi na hivyo kumpa msomaji fursa ya kuuelewa moja kwa moja.

Aidha, hadihi hizi zinaashiria masuala ibuka yanayomkabili binadamu katika harakati zake za kila siku. Bila shaka diwani hii ni mchango mkuu katika ufundishaji wa utanzu wa hadithi fupi.

Mkusanyiko huu umeteuliwa na kuwa kitabu cha fasihi cha Kiada katika Vyuo vya Ualimu Nchini kuanzia Septemba 2017

Vazi-la-mhudumu-cover-front-back