Msururu wa Makumba ni novela tano za sayansi ambazo zimechapishwa na Queenex Publishers mwaka 2018. Novela hizi zinahusu safari za kisayansi za mhusika Makumba na babu yake wakitalii sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu, mimea, anga na nyinginezo kwa kutumia GAJABU. Novela zenyewe ni

  1. MAKUMBA KATIKA SAFARI YA TONGE
  2. MAKUMBA NA SELIDAMU NYEUPE
  3. MAKUMBA NA MAJANABI
  4. MAKUMBA KATIKA SAFARI YA MAWIMBI
  5. MAKUMBA KATIKA SIRI YA MWEMBE

Tangazo La Mauzo Maalum Ya Novela Za Msururu Wa Makumba

MAKUMBA KATIKA SAFARI YA TONGE

Makumba na babu yake wanajikuta ndani ya mdomo wa nyanya kwa bahati mbaya. Na safari ya kulifwata tonge la chakula ikaanza bila ya wao kutarajia. Je walifanikiwa kutoka nje au walimeng’enywa tumboni?

MAKUMBA NA SELIDAMU NYEUPE

Makumba na babu yake waliingia kwenye mishipa ya damu ya nyanya ili kupigana na vimelea wa malaria. Lakini walipofika kule ndani walinaswa na kushikwa na selidamu nyeupe. Je watafanikiwa kupigana na vimelea wa malaria na kumponya nyanya aliyekuwa mahututi? 

 

MAKUMBA NA MAJANABI

Makumba, babu na nyanya walijipata wametekwa nyara na majanabi. Safari yao ya kujikomboa iliwapeleka kwenye sayari zote walizozijua. Je hatima yao ilikuwaje? 

 

MAKUMBA KATIKA SAFARI YA MAWIMBI

Makumba aliamua kusafiri peke yake na kuingia sikioni mwa babu ili alitalii na gajabu. Je alifanikiwa katika safari yake ama alibaki mwilini mwa babu?

 

MAKUMBA KATIKA SIRI YA MWEMBE

Makumba, babu na nyanya walitekwa nyara na Profesa Madevu na kuingizwa mwembe na kuachwa wafe mle ndani. Je walifanikiwa kutoka mwembeni?  Je Makumba aligundua siri gani ya Mwembe?

 

 

 

Tangazo La Mauzo Maalum Ya Novela Za Msururu Wa Makumba