NURU YA KIZA ni tamthilia ya Kiswahili. Imechapishwa mwaka 2016 na shirika la EAEP. Inahusu Mkulu kabaila Kabwela. Kabaila Kabwela (KK) ni Mkulu wa nchi ya Matopeni.

Siku moja anaamua kutathmini utendakazi wa maliwali wake aliowapa majukumu mbalimbali ya uongozi nchini. Jambo la kushangaza ni kuwa, mbinu aliyotumia kutathmini utendakazi wao ilikuwa ya ajabu sana.

Mbinu ambayo itamwacha kinywa wazi na kumduwaza msomaji wa tamthilia hii asithubutu kuiweka chini hadi tamati. Mbinu hiyo inadhihirisha kiwango cha juu cha ubunifu alichotumia mwandishi kufikisha ujumbe wake kwa wasomaji.

Nuru ya Kiza ni tamthilia ambayo inaakisi matatizo halisi yanayozikumba nchi nyingi barani Afrika. Matatizo ambayo yanasababishwa na ubinafsi na utepetevu wa viongozi wa nchi.

Babusa-nuru-ya-kiza-16