Warsha-ya-pili-ya-waandishi-wa-Kiswahili

Warsha ya pili ya waandishi wa Kiswahili itakuwa Jumamosi tarehe 20 Agosti kutoka saa mbili na nusu asubuhi kwenye shirika la Storymoja, mtaa wa Westlands. Kujisajili tuma shilingi 500 tu kwa TILL NUMBER 779741 au MPESA kwa 0728010459 simu yangu. Hifadhi ujumbe wako. Mada mbalimbali katika uandishi wa kubuni zitajadiliwa na vyeti kutolewa baada ya warsha. wakufunzi ni Rebecca Nandwa  Fred Obondo nami Hamisi Babusa.Wale waandishi ambao baada ya warsha wataweza kuandika miswada mizuri, basi kazi zao zitapokelewa na Storymoja na kuchapishwa. Shirika la Storymoja liko Westands, barabara ya Shanzu. Panda matatu nambari 119 steji ya Koja Mosque. teremka steji ya TOTAL na Barabara ya Shanzu, Lango la Pili lililo na rangi ya waridi (pink) ni Shirika la Storymoja. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Rebecca Nandwa 0725930221, Fred Obondo 0727163459 au mimi kwa nambari 0728010459. Wale ambao tayari wamelipa, karibuni. Wale ambao bado, msikose fursa hii ya kujiendeleza